Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 21:18

Arabian Gulf ya Libya imeanza tena uzalishaji mafuta wa ndani ya nchi


Mfano wa maeneo yenye mabomba ya mafuta nchini Libya.
Mfano wa maeneo yenye mabomba ya mafuta nchini Libya.

Kuanza tena uzalishaji wa kiwango cha chini ya uwezo kamili unalenga kusambaza umeme na mafuta kwa mahitaji ya ndani

Kampuni ya mafuta ya Arabian Gulf ya Libya imeanza tena uzalishaji hadi mapipa 120,000 kwa siku kukidhi mahitaji ya ndani, wakati mauzo ya nje bado yamesimamishwa, wahandisi walisema leo Jumapili, baada ya mvutano kati ya makundi hayo na kupelekea kufungwa kwa vinu vingi vya uzalishaji mafuta nchini humo.

Siku ya Jumamosi, Kampuni ya mafuta ya Arabian Gulf, mwendeshaji wa vinu vya mafuta vya Sarir, Messla na Nafoura nchini Libya ilitoa maelekezo ya kuanza tena uzalishaji.

Kuanza tena kwa uzalishaji ulio wa kiwango cha chini ya uwezo kamili wa viwanda, unalenga kusambaza umeme na mitambo ya mafuta kwa mahitaji ya ndani, wahandisi hao waliliambia shirika la habari la Reuters. Walizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina kwa sababu hakuna mamlaka ya kuzungumza hadharani.

Makundi huko mashariki mwa Libya, ambako uzalishaji wa mafuta upo juu, walifunga uzalishaji mwezi Agosti baada ya makundi makubwa Magharibi mwa Libya yalipomuondoa madarakani gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Libya

Sadiq al-Kabir, na nafasi yake kuchukuliwa na mtu kutoka bodi ya upinzani.

Forum

XS
SM
MD
LG