Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema wafanyakazi wa afya wanahitaji kutembea bila vikwazo ndani ya Gaza ili kusimamia chanjo, akisema kwamba usitishaji wa mapigano, hata kwa siku chache, itakuwa ni muhimu kulinda watoto wa Gaza kwa kupata chanjo za kawaida.
“WHO inatuma zaidi ya chanjo milioni moja za polio ambazo zitatolewa katika wiki zijazo,” aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.
Kugunduliwa kwa polio katika maji machafu huko Gaza ni ishara tosha kwamba virusi hivyo vimekuwa vikizunguka katika jamii, hivyo kuwaweka watoto ambao hawajachanjwa hatarini amesema.
Hakuna kesi za kliniki zilizo gundulika.
Forum