Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:34

Mji wa Sydney unaelekea kumaliza kabisa maambukizi ya HIV


Vipimo vya HIV
Vipimo vya HIV

Watafiti wamesema kwamba wilaya zilizo katikati mwa Sydney zinakaribia kuwa sehemu za kwanza duniani kufikia lengo la Umoja wa Mataifa, la kumaliza kabisa maambukizi ya virusi vya Ukimwi – HIV.

Kuna wakati mmoja Sydney ilikuwa mji wenye viwango vya juu vya maambukizi ya HIV nchini Australia lakini maambukizi mapya kati ya wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, yamepungua kwa asilimia 88 kati ya m waka 2010 na 2022.

Lengo la Umoja wa Mataifa ni kupunguza maambukizi ya HIV kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2030.

Visa 11 pekee vya maambukizi ya HIV viliripotiwa katikati mwa Sydney mwaka uliopita.

Karibu kila mtu nchini Australia, aliyeambukizwa HIV anapokea dawa za ARV kupunguza makali ya virusi hivyo.

Watu wengi ambao hawajaambukizwa HIV wanatumia dawa za kuzuia au kupunguza maambukizi iwapo wanafanya ngono na mtu aliyeambukizwa.

Forum

XS
SM
MD
LG