Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:19

Netanyahu, Gantz bado hawajakubaliana kuunda serikali ya mseto


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akihutubia katika tafrija ya kumkumbuka marehemu Rais Shimon Peres, huko Jerusalem, Septemba 19, 2019. Pia alitoa wito kwa mpinzani wake Gantz kuungana pamoja kuunda serikali ya umoja.(Photo by GIL COHEN-MAGEN / AFP)
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akihutubia katika tafrija ya kumkumbuka marehemu Rais Shimon Peres, huko Jerusalem, Septemba 19, 2019. Pia alitoa wito kwa mpinzani wake Gantz kuungana pamoja kuunda serikali ya umoja.(Photo by GIL COHEN-MAGEN / AFP)

Wakati hadi hivi sasa hakuna aliyeibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa Israeli, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu Alhamisi amemtaka mpinzani wake mkuu Benny Gantz washirikiane kuunda serikali ya mseto.

Katika ujumbe wa picha za video, Netanyahu amesema ni matumaini yake ya kuunda serikali ya mrengo wa kulia hayapo tena kutokana na matokeo ya uchaguzi.

Ametoa wito wa kumtaka Gantz ashirikiane naye mara moja ili kuunda “serikali pana ya umoja wa kitaifa.”

Gantz mwenye mrengo wa kati wa chama cha Blue and White, amesema hatoungana kuunda serikali ya umoja muda wa kuwa Netanyahu atabakia kuwa mkuu wa chama cha Likud. Msemaji mmoja amesema Gantz atatoa tamko lake baadae Alhamisi.

Pande zote zilishindwa kupata viti 61 vinavyohitajika kuunda serikali ya waliowengi katika Bunge lenye viti 120, ingawaje chama cha Blue and White kilipata viti viwili zaidi ukilinganisha na viti walivyopata chama cha Likud.

Avigdor Lieberman anaonekana ni mwenye nafasi yenye nguvu zaidi kutokana na kukosekana chama cha waliowengi. Lieberman, mkuu wa chama kinachojulikana kama Yisrael Beytenu (Israel ni Nyumbani Kwetu) amerejea mara kadhaa kusema anapendelea kuwepo serikali ya umoja ambayo itamaanisha serikali itakayo kuwa na chama cha Gantz cha Blue and White, Chama cha Netanyahu Likud, na chama chake yeye mwenyewe.

XS
SM
MD
LG