Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 09:37

Netanyahu na hasimu wake Gantz bado hawana kura za kutosha kuunda serikali


Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Waziri wa zamani wa Ulinzi Benny Gantz

Wakati kura zikiendelea kuhisabiwa Jumatano, vyama vikuu viwili vya Israeli havijaweza kupata kura za kutosha kuunda serikali ya waliowengi kwa kupata viti 61 katika bunge lenye viti 120.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa chama cha Likud hakujitangazia ushindi wala kukubali kushindwa wakati alipozungumza na wafuasi wake mapema Jumatano.

Amewaambia kuwa atafanya bidii zote kuunda serikali madhubuti yenye mrengo wa kizayuni ambayo itawatenga Waarabu.

Mpinzani wake na mkuu wa zamani wa jeshi la Israeli Benny Gantz, wa chama cha Blu na Nyeupe amesema mbele ya wafuasi wake waliokuwa wakimshangilia kwamba atajaribu kuunda serikali yenye sura ya muungano.

Muungano huo utakuwa ukielezea utashi wa wananchi. Mara tu baada ya kura za mwisho kutangazwa, Rais Reuven Rivlin atafanya mazungumzo na wakuu wa vyama vyote na kuwasihi Netanyahu na Gantz kuunda serekali.

Kiongozi mwenye ushawishi mkubwa hivi sasa, kama ilivyokuwa uchaguzi wa awali, ni Waziri wa Ulinzi wa zamani Avigdor Lieberman, ambaye anaungwa mkono zaidi na Chama cha Warusi cha Yisrael Beitenu.

Yeye anapendelea serikali ya umoja wa kitaifa ikiwemo chama la Likud cha Netanyahu, Gantz Blue and White na chama chake bila ya chama cha Ultra-orthodox au vyama vingine vidogovidogo.

Baada ya uchaguzi uliopita, Gantz alisema atafikiria aina hii ya serikali iwapo tu Netanyahu ataachia madaraka kama kiongozi wa chama cha Likud. Netanyahu anakabiliwa na madai ya ufisadi, ikiwemo wizi na kuvunja uaminifu.

Netanyahu alikuwa na matarajio ya kupata kura za waliowengi na wengi walitarajia baada ya hapo atajiwekea kinga asishtakiwe.

Yossi Klein Halevi wa Taasisi ya Shalom Hartman huko Jerusalem alisema uchaguzi huo ni kati ya wale wanaomuunga mkono Netanyahu na wale wanaompinga.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG