Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:34

Mke wa Waziri Mkuu wa Israel atozwa faini kwa kufuja fedha za serikali


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mkewe Sara
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mkewe Sara

Mke wa waziri mkuu wa Israel amehukumiwa kulipa faini ya takriban Dola za Marekani 15,000 kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Jerusalem Jumapili ilikubali ombi la makubaliano alilosaini Sara Netanyahu na waendesha mashtaka kufikia makubaliano juu ya madai ya kuwa alifuja fedha za serikali kiasi cha dola za Marekani 100,000 kwa kuzitumia kununua vyakula vya kifahari.

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka imesema kuwa mke wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu atalipa faini ya ziada ili kuhitimisha kesi hiyo, ambayo ili mtuhumu kwa kulipa bili za gharama ya juu za vyakula katika migahawa wakati makazi yake rasmi yalikuwa na mpishi aliyeajiriwa na serikali kutoa huduma kila siku.

Sara Netanyahu alikutikana ana kesi ya kujibu ya udanganyifu na kuvunja uaminifu mwaka 2018. Makubaliano hayo ya kumaliza kesi yalipelekea yeye kukiri tuhuma za makosa mengine madogo madogo na kupunguza kiwango cha matumizi yaliyovuka kiwango kufikia dola 50,000.

Kwa upande wake waziri mkuu anakabiliwa na kesi ya kujibu katika mashtaka tofauti ya ufisadi.

XS
SM
MD
LG