Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 06:18

Netanyahu asema anahakika nchi nyingine zitaiiga Marekani


Waandamanaji wa Palestina wakirusha bomu la machozi baada ya kupigwa na vikosi vya Isreali kufuatia maadamano yaliyosababishwa na uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, yaliyotokea Disemba 7, 2017.
Waandamanaji wa Palestina wakirusha bomu la machozi baada ya kupigwa na vikosi vya Isreali kufuatia maadamano yaliyosababishwa na uamuzi wa Rais Donald Trump kuitambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, yaliyotokea Disemba 7, 2017.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Alhamisi hana shaka kuwa nchi nyingine zitafuata nyayo za Marekani katika kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Amesema kuwa Marekani itapohamisha ubalozi wake Jerusalem nchi nyingine zitafanya hivyo pia.

Netanyahu amesema nchi yake inaendelea kuwasiliana na mataifa mengine lakini hakuzitaja nchi hizo, wakati akitoa hotuba yake katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel.

Jeshi la Israel limetangaza kuongeza vikosi zaidi kwenye Ukingo wa Magharibi ikiwa ni sehemu ya kile walichokiita “kuwa tayari kukabiliana na matukio yoyote.”

Uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kubadilisha sera ya Marekani ya miongo mingi juu ya suala la Jerusalem na kuanzisha harakati za mchakato wa kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv umepingwa vikali na viongozi wa Palestina.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema mpango wa Trump umeifanya Marekani kupoteza nafasi yake ya usuluhishi katika kutafuta amani.

Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh ametaka kuwepo kwa mandamano ya Wapalestina yanayojulikana kama intifada, au muamko wa kupinga Israel kuanzia Ijumaa.

“Tunataka maadamano haya yadumu na kuendelea ili kumfanya Trump na wanaokalia ardhi ya Palestina wajute kwa kufanya uamuzi huu,” Haniyeh amesema Alhamisi alipokuwa anatoa hotuba huko Gaza.

XS
SM
MD
LG