Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 19:10

Viongozi mbalimbali wa dunia wampongeza Netanyahu


Waziri Mkuu wa Israel akiwahutubia wafuasi wake wa chama tawala cha Likud huko Tel Aviv Aprili 10, 2019, baada ya matokeo ya awali kuonyesha ushindi wake bungeni.

Salamu za pongezi kutoka kwa viongozi mbalimbali duniani zimeendelea kumiminika kwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu baada ya kuibuka kidedea kwa mara nyingine katika uchaguzi wa bunge kwa muhula mpya wa uongozi.

Hadi Jumatano asilimia 97.4 ya kura zikiwa zimehisabiwa, matokeo ni kuwa chama cha Likud cha Netanyahu na washirika wake wa kisiasa kimepata ushindi wa viti 65 vya bunge la Israel lenye viti 120. Vyanzo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa Alhamisi mchana.

Katika ujumbe wa pongezi kwa Netanyahu Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuchaguliwa tena kwa kiongozi huyo ni ishara nzuri ya amani. Trump ameeleza hayo akiwa mjini Washington wakati wa mkutano wake na waandishi habari.

Vyanzo vya habari vimeongeza kuwa Kansela wa Austria Sebastian Kurz na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ni kati ya viongozi wa kwanza kutuma salamu hizo za pongezi kwa Netanyahu.

Kurz amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na Netanyahu katika siku za usoni kwa maslahi ya watu wa Israel na Austria.

Katika ujumbe wake kwenye ukurasa wa Twitter, Waziri Mkuu Modi amemuelezea Netanyahu kuwa ni rafiki mkubwa wa India.

Ameahidi kuwa India itaendelea kushirikiana naye kwa lengo la kuufikisha mbali uhusiano ulioko kati ya nchi hizo mbili.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffan Seibert amesema nchi hiyo inasubiri matokeo rasmi ya uchaguzi huo uliofanyika jana Jumanne

Katika tamko lake imesema kuwa iko tayari kufanya kazi na serikali mpya ya Israel kwa ushirikiano wa karibu.

Nchi hiyo imesisitiza kuwa uhusiano uliopo kati ya mataifa hayo mawili, licha ya kuhitalafiana katika juu ya sera ya Israel ya makaazi ya hivi karibuni.

.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG