Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 05:06

Mueller: Uchunguzi haukumsafisha Trump na madai ya kuzuia sheria


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Mwendesha mashtaka wa zamani Robert Mueller ameliambia Baraza la Wawakilishi Jumatano kwamba uchunguzi dhidi ya Russia kuingilia uchaguzi wa rais wa Marekani 2016 haujamsafisha Rais Donald Trump juu ya shutuma za kuzuia sheria kufuata mkondo wake kwa kujaribu kuzuia uchunguzi, ijapokuwa kiongozi wa Marekani amekuwa akidai hilo.

Wakati muda wa mahojiano hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Baraza la Wawakilishi Jerrold Nadler alimuuliza mwendesha mashataka huyo, “Je, ulimsafisha kikamilifu Rais?”

Mueller alijibu “hapana” baadae na kuongeza, “Rais hakusafishwa kwa vitendo inavyodaiwa alivitenda.

Mueller alieleza, hata hivyo, kuwa Trump hakuweza kufunguliwa mashtaka ya jinai kwa sababu ya sera ya muda mrefu ya Wizara ya Sheria inayokataza kumfungulia mashtaka rais aliyeko madarakani.

Mueller amesema timu yake bila ya mafanikio kwa mwaka mmoja imejaribu kufikia makubaliano na Trump ili atoe maelezo ana kwa ana, lakini rais amejibu tu maswali kwa maandishi.

Baadae katika mahojiano hayo, Mwakilishi wa Republikan Ken Buck alimuuliza Mueller, “ Je, unaamini kuwa yeye amefanya makosa --- ungeweza kumfungulia mashtaka rais wa Marekani kwamba alizuia sheria isichukue mkondo wake baada ya kumaliza muda wake wa urais? Mueller alijibu “ndiyo.”

Kwa nini Trump hakushtakiwa

Hata hivyo, Mueller akifupisha ripoti ya uchunguzi wake kufikia takriban kurasa 448 baada ya miezi 22 ya uchunguzi, alikiri kwa Mwakilishi wa Republikan Doug Collins kuwa wachunguzi wake walitoa hitimisho kuwa haukuwepo ushahidi wa kutosha kumfungulia mashtaka Trump au wafanyakazi wa kampeni yake ya 2016 walihusika na hujuma ya kushirikiana na Russia kumsaidia Trump kushinda kutumikia kipindi cha urais cha miaka minne Ikulu ya White House.

Mwakilishi mwengine wa Republikan, James Sensenbrenner, alimkosoa Mueller kwa kuendelea na uchunguzi dhidi ya Trump hata baada ya kujua kuwa Trump asingeweza kufunguliwa mashtaka kwa makosa ya jinai, ingawaje Mueller alisema kufanya hivyo ni ruhsa chini ya muongozo wa Wizara ya Sheria.

“Kama huwezi kumfungulia mashtaka rais, kwa hiyo utaendelea kutafuta makosa, hayo ndiyo maoni yangu,” Sensenbrenner amesema.

Wakati Kamati ya Sheria ya Baraza la Wawakilishi ikimaliza mahojiano hayo ya masaa matatu na nusu, Msemaji wa Ikulu ya White House Stephanie Grisham amesema, “Masaa matatu ya mwisho yamekuwa ni fedheha kubwa kwa Wademokrat. Tegemeni zaidi ya hayo katika sehemu ya pili ya mahojiano hayo.

Hitimisho la Mueller katika mahojiano

Watunga sheria ndani ya Kamati ya Usalama ya Baraza la Wawakilishi walimuuliza Mueller juu ya aliyogundua kuhusiana na namna Russia ilivyoingilia kati uchaguzi ili kumsaidia Trump kumshinda Hillary Clinton, hasimu wake katika uchaguzi wa 2016.

Trump mara nyingi amekuwa akishambulia kwa maneno uchunguzi wa Mueller, lakini Mueller ametupilia mbali mara kwa mara madai yake rais, kwa kusema, “uchunguzi huu siyo kwa ajili ya kumtafuta mchawi,”

Mueller amejibu maswali mengi akitumia majibu mafupi ya kushangaza ya ndiyo au hapana, akisema anasimama imara kwa hitimisho lilioko katika ripoti yake ndefu. Wakati fulani alisema, “Mara nyingine rejeeni kwenye ripoti,” na kukataa kufanya uchambuzi zaidi juu ya yale aliyoyagundua katika uchunguzi wake.

XS
SM
MD
LG