Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:45

Wananchi wa Marekani watoa maelezo juu ya mteule wa Trump


Mtu anayepinga uteuzi wa Brett Kavanaugh akamatwa wakati Brett Kavanaugh akitoa maelezo yake mbele ya Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti Washington, DC.
Mtu anayepinga uteuzi wa Brett Kavanaugh akamatwa wakati Brett Kavanaugh akitoa maelezo yake mbele ya Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti Washington, DC.

Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti itasikiliza maelezo Ijumaa kutoka kwa watu ambao wanamfahamu mteule wa nafasi ya Mahakama ya Juu Brett Kavanaugh.

Kavanaugh alimaliza siku ya tatu ya mahojiano Alhamisi, siku moja baada kudai yeye ni mtu huru kama jaji, lakini akakataa kushinikizwa kujibu maswali yanayo husiana na uchunguzi dhidi ya Rais Donald Trump.

“Mimi ni jaji niliye na uhuru wangu,” Kavanaugh mwenye umri wa miaka 53 ameiambia Kamati ya Sheria ya Baraza la Seneti. “Mimi ninawajibika kwa Katiba ya nchi, na Katiba ndiyo inanifanya mimi niwe jaji huru, ambaye nalazimika kufuata sheria kama zilivyoandikwa.

Lakini Kavanaugh alikataa kueleza msimamo wake iwapo rais anaweza iwapo rais anaweza kuitwa na mahakama na kujibu maswali, iwapo rais anaweza kutoa msamaha wake binafsi anapokuwa ametuhumiwa kuvunja sheria, na iwapo bado anaamini, kama alivyo andika miongo miwili iliyopita, kwamba rais anaweza kumfukuza mwendesha mashataka anaye mchunguza.

Maswali yanayo husiana na uchunguzi unaoendelea ambao unafanywa na mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller kuangalia iwapo kampeni ya Trump ili shirikiana na Russia kumsaidia kushinda uchaguzi na iwapo Trump, kama rais, alizuia sheria isifuate mkondo wake kwa kujaribu kuingilia kati uchunguzi.

Siku ya Alhamisi, Kavanaugh alikabiliwa na maswali mapya juu ya maoni yake ya uamuzi wa Mahakama ya Juu 1973 iliyo idhinisha haki ya kutoa mimba nchini Marekani, na kusema anaamini uamuzi huo ni sheria iliyokuwa tayari imepitishwa na ilikuwa imesisitizwa katika maamuzi mengi ya hivi karibuni.

Lakini Kavanaugh alikataa kutoa maoni yake iwapo anafikiri uamuzi huo ulikuwa umefanyika sawa sawa kutokana na msimamo ya kisheria. Makundi mbalimbali ya wanawake yanapaza sauti zao kupinga kuteuliwa kwa Kavanaugh, wakihofia kuwa atatoa kura ya tano muhimu inayohitajika katika Mahakama ya Juu akiungana na majaji wanne wengine wenye misimamo ya kikonservative kuwezesha mahakama kubadilisha uamuzi wa utaoji mimba au kuzuia wanawake kuweza kupatiwa utaratibu huo wa utaoji mimba.

Trump, ambaye alimteua Kavanaugh Julai, amesema Jumatano kuwa anaridhika na utaratibu wa mahojiano unavyoendelea, akisema Kavanaugh alikuwa ametoa majibu ya kina kwa maswali magumu.” Kiongozi huyo wa Marekani amemtaja Kavanaugh “kuwa jaji wa kipekee” ambaye “alizaliwa kwa ajili ya kutumikia nafasi hiyo.”

Kavanaugh amesema wazi “hakuna mtu aliyekuwa juu ya sheria katika mfumo wetu wa katiba” na kuwa “haijalishi ni wapi upo katika maisha, haijalishi nafasi ulionayo katika serikali, haki ni kwa wote chini ya sheria.” Lakini alikataa kusema iwapo rais aliyeko madarakani, kama raia wengine wote, analazimika kuitikia wito wa mahakama kutoa maelezo yake.

“Siwezi kuwapeni majawabu kwa swali hilo la kufikirika.” Mteule huyo alisema.

XS
SM
MD
LG