Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:27

Muigizaji Burt Reynolds, aaga dunia akiwa na umri wa miaka 82


Burt Reynolds
Burt Reynolds

Muigizaji nyota wa filamu, Burt Reynolds, mwenye mvutio wa kipekee na aliyeweza kutumikia fani yake kwa zaidi ya nusu karne, amefariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 82.

Wakala wake ametangaza kifo cha mwigizaji huyu huko mjini Jupiter, Florida, lakini hakutoa sababu za kifo chake.

Mwigizaji Reynolds, machachari na mwenye haiba, alikuwa ni mfano wa kiugwa katika miaka ya 70 na pia kipenzi cha watu maarufu Hollywood.

Reynolds ambaye alizaliwa Michigan na kuwa nyota wa mpira wa football wakati akiwa mwanafunzi katika moja ya vyuo vikuu Florida alionekana kuwa na mwelekeo wa kuingia katika michezo ya kulipwa kabla ya kujeruhiwa katika ajali ya gari.

Alifanya kazi mbalimbali kabla ya kuingia katika uigizaji huko Florida na New York na hatimaye akajiunga na Hollywood na kutumikia majukumu mbalimbali katika televisheni.

Umashuhuri wake mkubwa ulijitokeza mwaka 1972 aliposhiriki katika filamu iliyopata umaarufu ilioitwa Deliverance, ilikuwa ikizungumzia safari ya boti ambayo iligeuka kuwa hatari.

Filamu hiyo ilichaguliwa kwenye tuzo ya Academy kwa kuwa na sifa ya Picha Bora, na nafasi aliyocheza Reynolds ilisifiwa na wengi.

XS
SM
MD
LG