Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 14:02

Mueller asema muongozo haukumruhusu kumshtaki Trump


 Rais Donald Trump (kulia), Robert Mueller
Rais Donald Trump (kulia), Robert Mueller

Mwendesha mashtaka maalum nchini Marekani, Robert Mueller, alisisitiza Jumatano kuwa kumfungulia mshtaka Rais Donald Trump kwa tuhuma za kuzuia sheria kufuata mkondo wake siyo hatua ambayo ofisi yake ingefikiria kuchukua chini ya mwongozo wa sera za Idara ya Sheria.

Amesema hayo wakati akitangaza kufungwa kwa ofisi yake baada ya kuhitimisha mwisho wa mwezi Machi uchunguzi uliochukua miezi 22 juu ya Russia kuingilia kati uchaguzi wa urais wa Marekani 2016 na uwezekano kwamba Trump alizuia sheria isifuate mkondo wake.

Akieleza sera ya muda mrefu ya Idara ya Sheria kuwa rais aliyeko madarakani hawezi kushtakiwa, Mueller aliwaambia waandishi katika maelezo yake ya kwanza kwa umma : "Hivyo kumshtaki Rais kwa kosa la jinai siyo kitu ambacho tungeweza hata kukifikiria.”

Amesema kuwa itakuwa sio “haki kumtuhumu mtu kwa kosa wakati hakuna azimio la mahakama kwa shtaka linalohusika.”

Lakini pia aliongeza kuwa “Ingekuwa tuna uhakika kuwa rais hakutenda kosa la jinai, tungesema hivyo.”

Mwendesha mashtaka huyo maalum alitangaza kuwa anajiuzulu kutoka Idara ya Sheria akirejea uraiani ili kuishi maisha yake binafsi.

Mueller alikuwa mshirika wa Kampuni ya mawakili ya WilmerHale, Washington, D.C kabla ya kuchaguliwa kuwa mwendesha mashtaka maalum kuichunguza Russia mwezi Mei 2017.

Alikuwa amehitimisha Ripoti ya siri yenye kurasa 448 juu ya uchunguzi huo aliyoituma kwa Mwanasheria Mkuu William Barr akieleza kwamba hakuna ushahidi kwamba kampeni ya Rais Trump ilishirikiana na Moscow katika vitendo vya uhalifu.

Lakini suala la iwapo Trump alizuia uchunguzi usifanyike, mwendesha mashtaka maalum amesema kwa kuwa hangeweza kupendekeza kufunguliwa mashtaka ya kidesturi dhidi ya Trump, pia hakuweza kumwondolea lawama Trump kwamba hakuwa makosa.

Alielezea matukio 11 ambayo huenda yakawa ni vitendo vya kuzuia sheria kuchukua mkondo wake.

XS
SM
MD
LG