Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 16:38

Trump ashtushwa na hatua ya Warepublikan kumhoji mwanawe


 Donald Trump Junior
Donald Trump Junior

Rais wa Marekani Donald Trump, amesema alishtushwa sana na hatua ya kamati ya upelelezi katika baraza la seneti, linaloongozwa na Warepublican, kumtaka mwanawe mkubwa wa kiume, Donald Trump Junior, kufika mbele yake kuhojiwa.

Mtoto wa Trump ametakiwa kutoa maelezo zaidi kuhusiana na madai ya Russia kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016.

Haijajulikana iwapo Trump Junior atafika mbele ya kamati hiyo kwa mahojiano licha ya kutakiwa kufanya hivyo na kamati inayoongozwa na Warepublican.

Uchunguzi wa mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller, ulimwondolea Rais Trump madai ya kampeni yake kushirikiana na Russia kumsaidia kushinda urais.

Mueller hata hivyo hakufikia maamuzi ya kumfungulia mashtaka Trump, katika madai ya kuwa alijaribu kuzuia sheria isifuate mkondo wake kwa kujaribu kuzuia uchunguzi wa Russia kufanyika.

Hata hivyo Mwanasheria Mkuu William Barr, aliamua kwamba hakuna haja ya kumfungulia Trump mashtaka yoyote.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG