Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:42

Ripoti ya Mueller: Kampeni ya Trump haikushirikiana na Russia


Mwendesha mashtaka maalum wa Marekani, Robrt Mueller.
Mwendesha mashtaka maalum wa Marekani, Robrt Mueller.

Baada ya takriban miaka miwili ya uchunguzi wa kina kuhusu iwapo Rais Trump au wafanyakazi katika kampenmi yake walishirikiana na Russia katika kuingilia kati uchaguzi wa urais wa mwaka 2016, hatimaye masuala muhimu kwenye ripoti ya mwendesha mashtaka maalum, Robert Mueller, yaliwekwa wazi Jumapili.

Hii ni kufuatia vuta nikuvute ambayo imeleta msisimko mkubwa wa kisiasa nchini Marekani.

Baada ya kupokea ripoti hiyo kutoka kwa Robert Mueller siku ya Ijumaa, Mwanasheria mkuu wa Marekani, William Barr, alituma barua kwa bunge Jumapili, iliyoeleza, kati ya mengine, kwamba uchunguzi huo haukuonyesha ushirikiano wowote kati ya Wamarekani na Warussia kuhusiana na suala hilo.

"Uchunguzi haukubaini ushirikiano wowote kati ya Rais Trump, au wafanyakazi katika kampeni yake, na Russia. Hata hivyo, licha ya kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha Rais Trump alikuwa kuzingiti kwa sheria kuteneka, uchunguzi huo haukupata ushahidi kwamba Trump hakuwa na hatia," ripoti hiyo ya kurasa nne ilieleza.

Rais wa Marekani Donald Trump awasili kwenye bustani za Ikulu mjini Washington DC baada ya ripoti ya Mueller kutolewa.
Rais wa Marekani Donald Trump awasili kwenye bustani za Ikulu mjini Washington DC baada ya ripoti ya Mueller kutolewa.

Mengine muhimu ni kwamba uchunguzi huo ulibaini bila tashwishi kuwa Russia iliingilia kati uchaguzi huo.

Jambo la tatu lililofichuliwa na uchunguzi wa Mueller ni kwamba Zaidi ya watu 2,800 walihojiwa wakati wa mchakato huo.

Barua hiyo pia ilieleza kwamba ripoti ya kina kutoka kwa mwendesha mashtaka maalum itatolewa hivi karibuni.

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Prof Fulbert Namwamba, aliiambia Sauti ya Amerika kwamba kuwasilisha ripoti hiyo kwa mwanasheria mkuu ni mwanzo tu wa mchakato mwingine mrefu kwelekea kwa uchaguzi wa 2020.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr
Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr

"Licha ya ripoti hiyo kueleza hakuna ushirikiano na Warusi, nawahakikishia kwamba huu ni mwanzo tu kwani kuna wadau wengi ambao hawajatosheka na watafanya juu chini katika upoekuzi wao. Hivyo ndivyo zilivyo siasa za Marekani," alisema Namwamba.

Uchunguzi huo ulianza Mei 17, 2017 baada ya naibu wa Mwanasheria Mkuu Rod J. Rosenstein kumteua Mueller kufuatia hatua ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions kutangaza kwamba hangeshiriki kwa lolote kuhusu uchunguzi huo.

Hatua hiyo ilifuatia shinikizo kadhaa hususan kutoka kwa Wademokrat wakimtaka ajiondoe.

XS
SM
MD
LG