Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 15:35

Mkutano wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuanza Jumatatu Zanzibar


Fukwe za Kisiwa cha Zanzibar

Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA) unatarajiwa kuanza Jumatatu mjini Zanzibar.

Taarifa ya mkutano huo inaeleza mkutano huo ni muhimu kwani utawaweka pamoja Maspika, Naibu Maspika na wabunge zaidi ya 400 kutoka nchi mbalimbali za Afrika. RAIS wa Zanzibar, Ali Muhamed Shein, anatarajiwa kufungua mkutano huo.

Akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya mkutano huo, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid, amesema kufanyika kwa mkutano huo Zanzibar ni fursa nzuri kwa wananchi wa Zanzibari na Tanzania kujitangaza katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kiuwekezaji.

Alifafanua kuwa maeneo hayo ni pamoja na utalii, biashara, diplomasia nauwekezaji, ambazo ni sehemu muhimu za kiuchumi.

Ameeleza fursa hiyo inatokana na ugeni huo wa mataifa zaidi ya 18 ambao wana ushawishi mkubwa katika masuala hayo ya kiuwekezaji, biashara na utalii katika nchi zao.

Baadhi ya nchi zitakazoshiriki mkutano huo ni Zambia, Ghana, Malawi, Nigeria, Cameroon, Afrika Kusini, Uganda pamoja na wenyeji Tanzania.

"Kuwapo kwa siku tano nchini kwetu ni wakati adhimu kwa ugeni huu kuona mandhari nzuri ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwani tuna vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini na sera na vivutio vya biashara na uwekezaji," amesema Maulid.

Spika huyo alieleza kuwa, wageni hao watakuwa mabalozi wazuri katika kutangaza utalii na kupeleka sifa ya visiwa vya Zanzibar ikiwemo mandhari mazuri.

Mwenyekiti wa kamati utendaji ya wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) kutoka Zanzibar, Simai Mohamed Said, amesema mkutano huo ni fursa nyingine ya kuitangaza Jamhuri ya Muungano pamoja na Zanzibar katika sekta ya utalii na uwekezaji.</p>

''Hii ni fursa nyingine ya kupokea idadi kubwa ya wageni ambapo safari hii watatembelea Zanzibar na kujionea vivutio vilivyopo pamoja na ukarimu wa wananchi wetu''alisema.</p>

Katika mkutano huo Tanzania ambayo ndiyo makao makuu ya (CPA) kanda ya Afrika itatumia fursa hiyo kuwashawishi wajumbe kuridhia kuwa sehemu ya kuwekeza katika ujenzi wa hoteli ya nyota tano katika makao makuu ya mji huko Dodoma.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG