Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 28, 2024 Local time: 18:58

Marekani, Uingereza zakerwa na ukandamizaji wa haki za kisheria Tanzania


Erick Kabendera akiwa mahakamani.
Erick Kabendera akiwa mahakamani.

Balozi za Marekani na Uingereza nchini Tanzania zimeeleza kusikitishwa na kuongezeka kubanwa kwa utaratibu wa haki za kisheria nchini humo, kufuatia matukio ya mara kwa mara ya raia kukamatwa na kuzuiliwa kwa muda mrefu bila kupelekwa mahakamani.

Serikali pia inakosolewa kwa kitendo cha mtu kubadilishiwa mashtaka na mamlaka za sheria, hali inayotoa wasiwasi mkubwa kwa mustakabali wa haki za binadamu nchini humo.

Aidha tukio la kukamatwa kwa Erick Kabendera, mwandishi wa habari anayeandikia vyombo vya habari ndani na nje ya nchi, katika mazingira ya kutatanisha, na mwenendo wa shauri lake kugubikwa na utata, balozi za Marekani na Uingireza zimeitaka serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la kuheshimu haki za kiraia.

Hii inatokana na Tanzania ilivyotambua kuwa haki za kiraia ni za msingi, pamoja na kuridhia mikataba mbalimbali ya haki za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, likiwemo azimio la kimataifa la haki za Rai na Kisiasa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG