Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:56

Chadema yataka wanachama wake wafikishwe mahakamani


Freeman Mbowe
Freeman Mbowe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimedai kuwa polisi wamekuwa wakiwasumbua wanachama wao na hakuna hatua yoyote ya kuwafikisha mahakamani inayochukuliwa.

Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vincent Mashinji amehoji ni kwa nini wale ambao tayari wameripoti polisi wasiambiwe makosa yao na kupelekwa mahakamani.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:12 0:00

Amesema wanachama wao wamekuwa wakiripoti polisi lakini hakuna kitu chochote kinachofanyika.

Wanachama wetu wamekuwa wakijitahidi kuripoti polisi siku zote lakini kama binadamu lazima ikubalike wanapokuwa wamepatwa na udhuru, ameongeza.

Pia ameeleza kuwa Jeshi hilo limejikita katika kuwasukuma wananchi na siyo kutoa huduma kwa wananchi.

Wakati huohuo Jeshi la Polisi linawasaka wabunge wa wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kutoripoti polisi wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Chadema wabunge hao wa upinzani ni Halima Mdee (Kawe) na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiku (Tarime Mjini) walishindwa kuripoti polisi wiki iliyopita kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za bunge vinavyoendelea mjini Dodoma.

Naye wakili wa Chadema, John Malya amesema kuwa mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika wamewekwa chini ya ulinzi kusubiri maelekezo ya kwa nini hawakuhudhuria wiki iliyopita.

“Wiki iliyopita Jumanne, wenzao waliripoti, lakini Heche na Mnyika hawakuripoti walikuwa bungeni, lakini leo wameripoti na sasa amekuja hapa Mkuu wa Upelelezi akasema mkae hapa msubiri maelekezo.

“Halima ameshindwa kuripoti, yuko nje kwa matibabu na sisi ndiyo tuko hapa tunasubiri hayo maelekezo.

Katika mwendelezo wa kuitikia wito wa kuripoti kituoni hapo, leo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji wameripoti.

Wengine waliofika kituoni hapo ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

XS
SM
MD
LG