Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:15

Jubilee yakiri kushirikiana na Cambridge Analytica


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akisimama mbele ya bango lililoandikwa jina la chama chake, Jubilee.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akisimama mbele ya bango lililoandikwa jina la chama chake, Jubilee.

Chama kinachotawala nchini Kenya, Jubilee, kilisema Jumanne kwamba  kiliilipa kampuni iitwayo SLC, iliyo na uhusiano na kampuni ya Cambridge anlytica (CA), ambayo imegubikwa na utata, kukifanyia matangazo na kukitafutia umaarufu wakati wa kampeni za chaguzi kuu mbili zilzizopita.

Naibu mwenyekiti wa chama hicho cha Jubilee, David Murathe, alinukuliwa na shirika la habari la Reuters akikiri kwamba kampuni hiyo ilihusika kukitafutia umaarufu chama hicho lakini hakutoa maelezo ya kina kuhusu mbinu zilizotumika.

Cambridge Analytica inashutumiwa kwamba ilihusika kwenye mzozo wa kupotosha watu na kutumia takwimu visivyo, ambao pia unaikabili kampuni ya Facebook.

Chaguzi zote mbili za Kenya za mwaka wa 2013 na 2017 ziligubikwa na utata, na kupelekea kesi tatu kuwasilishwa kwenye mahakama ya juu. Kati ya masuala yaliyozua utata ni matumizi ya mfumo wa kielektroniki uliotumiwa kwenye chaguzi hizo.

Shirika la habari la Channel 4 news la Uingereza, lilionyesha video iliyorekodia kwa siri, na kufichua kwamba kampuni ya CA ilihusika pakubwa kwenye kampeni za chaguzi hizo mbili za Kenya, chini ya ufadhili wa muungano wa kisisa wa wakati huo uliopewa jina la 'Jubilee'.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, CA ilichangia pakubwa ushindi wa rais Donald Trump kwenye uchaguzi wa Novemba mwaka wa 2016.

Kampuni hiyo imehusishwa na kashfa zingine mbalimbali, iikiwa ni pamoja na kukiri kwamba ilikuwa inawatumia makahaba kwenye baadhi ya michakato.

"Tunaweza kutuma wasichana nyumbani kwake ili kupata ushahidi wa kutumia dhidi yake," afisa mkuu wa kampuni hiyo, Alexander Nix, alisema kwenye video hiyo ya siri.

Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa Cambridge Analytica, Alexander Nix, ambaye alisimamishwa kazi tarejhe 20 mwezi Mach, 2018 kufuatia kashfa iliyoikumba kampuni hiyo.
Aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa Cambridge Analytica, Alexander Nix, ambaye alisimamishwa kazi tarejhe 20 mwezi Mach, 2018 kufuatia kashfa iliyoikumba kampuni hiyo.

​Nix, ambaye alionekana kwenye video hiyo ya siri akieleza jinsi walivyotumia mbinu zisizo halali katika utekelezaji wa kazi zao, alisimamishwa kazi siku ya Jumanne kufuatia kashfa hiyo na kampuni hiyo ikaeleza kwamba inafanya uvchunguzi kuhusu sakata hiyo.

Facebook tayari imesitisha uhusiano wake na CA na kuikataza kampuni hiyo kutumia mtandao huo kwa matangazo yake.

XS
SM
MD
LG