Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 16:06

Tanzania yataka uchunguzi wa mauaji ya askari wake


Miili ya wanajeshi 14 waliouawa DRC yaagwa nchini Tanzania.

Serikali ya Tanzania imeutaka Umoja wa Mataifa (UN) kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na shambulizi la waaasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) lililoua wanajeshi watanzania 14.

Wanajeshi hao wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (JWTZ) walikuwa katika kikosi cha ulinzi wa amani cha UN nchini humo huku wengine 44 wakijeruhiwa.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA anaripoti kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ndiye aliyeongoza maombolezo rasmi ya kuaga miili 14 ya askari wa jeshi hilo.

Sherehe hiyo ya kuwaaga ilifanyika makao makuu ya JWTZ jijini Dar es Salaam na baada ya hapo miili hiyo kupelekwa maeneo walikotoka ikiwemo miili tisa ambayo imesafirishwa kwenda visiwani Zanzibar.

Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi alisisitiza kuwa Tanzania haijakatishwa tamaa kwa tukio hilo la shambulizi na mauaji ya askari wa JWTZ huko DRC

Disemba 8, 2017, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa taarifa ya vifo vya askari hao ambao walikuwa nchini Kongo kulinda amani, huku arobaini na wanne wakijeruhiwa vibaya. Miili ya askari wa JWTZ ilirejeshwa nyumbani Tanzania Jumanne desemba 12 mwaka huu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG