Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 19:52

Maelfu ya mahujaji wa Kiyahudi wawasili Ukraine kuadhimisha mwaka mpya Rosh Hashana


Mahujaji kutoka Israeli wakiwa katika mji wa Uman, kilomita 200 (125 miles) kusini mwa mji mkuu wa Ukraine, Kiev, Ukraine, Jumapili, Sept. 25, 2022.

Maelfu ya mahujaji wa kundi la Kiyahudi la Hasidic wamewasili Ukraine ya kati  kuadhimisha mwaka mpya wa Wayahudi Jumapili, wakipuuzia onyo la kimataifa la kusafiri.

Russia imekuwa ikifanya mashambulizi ya angani katika meneo kadhaa zaidi inayoyalenga na kuhamasisha raia wake kukabiliana na hali ya kuemewa kutokana na vita vinayoingia mwezi wake wa nane.

Mahujaji hao, wengi wao wakitokea Israel na maeneo mengine, walikusanyika katika mji mdogo wa Uman, eneo alilozikwa Nachman wa Breslov, kasisi wa Hasidic anayeheshimiwa na aliyefariki mwaka 1810.

Barabara wa mtaa mmoja wa kati wa Uman zilikuwa zimefurika wanaume wa umri mbalimbali wakivaa makoti meusi vazi la utamaduni wao na nywele zinazoning’inia pembeni. Baadhi walikuwa wakipaza sauti katika maombi. Wengine walipiga makelele, na kucheza ngoma. Matangazo na alama zinazotoa maelezo katika lugha ya Hebrew zilikuwa kila pahali.

Baadhi ya wageni, kama Nahum Markowitz kutoka Israel, wamekuwa wakifanya safari hii kwa miaka kadhaa na hawakuwa tayari kuruhusu vita kuwazuilia mwaka huu.

“Sisi hatuongopi. Ikiwa tunakuja kwa Kasisi Nachman, atatulinda kwa mwaka mzima,” alisema Markowitz, ambaye amekuwa akizuru Uman tangu mwaka 1991, wakati Umoja wa Soviet ulipovunjika na kuwezesha wageni kuweza kufanya hija.

Mbali na hayo, alisema, yeye anauzoefu tayari wa hatari za vita na milio ya ving’ora ambavyo hutokea ukiwa unaishi Israeli.

Mji huo, ulioko kilomita 200 (maili 125) kusini mwa mji mkuu, Kyiv, unadesturi ya kuvutia maelfu ya mahujaji kwa ajili ya Rosh Hashana, mwaka mpya wa Kiyahudi, ambao unaanza jioni ya Jumapili na kumalizika Jumanne.

Ubalozi wa Ukraine nchini Israeli ulikariri kuwataka wale waliopanga kufanya safari kubaki nyumbani, ikiwaonya kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa Russia imeendelea kulenga mashambulio kwenye maeneo yenye watu wengi na kuwa “mashambulizi hayo yanasababisha hatari ya kweli kwa maisha yako!”

Serikali za Israeli na Marekani pia zimeonya raia kutosafiri mwaka huu kuelekea huko – na baadhi ya tahadhari hizo zimesaidia.

Zaidi ya mahujaji 35,000 walizuru mwaka jana licha ya kukabiliwa na katazo la kusafiri kutokana na janga la COVI-19, alisema afisa wa eneo Oleh Hanich.

Mwaka huu idadi ya walijitokeza kusafiri ni ndogo, lakini bado ni wengi, ukizingatia kuwa hakuna ndege ya abiria zinazowalisi nchini humo. Jamii ya Umoja wa Wayahudi wa Ukraine walisema mahujaji 23,000 walikuwa wamewasili Uman hadi siku ya Jumapili.

“Siyo virusi vya corona wala vita inaweza kuwazuia kuja. Kwa watu hawa, hili ni eneo takatifu,” Hanich alisema, huku akikiri “hatuwezi kudhamini kikamilifu usalama wao.”

Rav Mota Frank, 54, hapo awali alikuwa anasita kusafiri kutoka mwaka huu. Lakini aliamua ilikuwa inastahiki kukabiliana na hatari baada ya kugundua kuwa hali katika eneo Uman ni tulivu zaidi kuliko maeneo ya mstari wa mbele na baada ya kuona namna Waukraine walivyoonyesha ukakamavu kukabiliana na hatari za vita.

“Panapokuwa na milio ya ving’ora, hawajifichi katika eneo la nyumba chini ya ardhi, lakini wanajaribu kuwa karibu na eneo la hifadhi,” alisema kuhusu Waukraine. “Sisi huko Israeli tumezoea hili – pia tunavita inayoendelea. Tumezoea maisha ya namna hii. Ndio maana haituogopeshi sana.”

Uman kwa hakika iko mbali na mstari wa mbele wa vita upande wa mashariki na kusini ya Ukraine, lakini iko katika masafa ambayo makombora ya Russia yanaweza kufikia na imewahi kushambuliwa.

Mwaka 2020, maelfu ya mahujaji walishindwa kufika Uman baada ya Ukraine kufunga mipaka yake kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya COVID-19.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG