Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 21:41

Biden aangazia Ukraine, usalama wa chakula na afya ya dunia akihutubia Baraza Kuu la UN


World leaders address the 77th Session of the United Nations General Assembly at U.N. Headquarters in New York City
World leaders address the 77th Session of the United Nations General Assembly at U.N. Headquarters in New York City

Kwa kutofuata utamaduni wa marais wa Marekani, Joe Biden hakuongea siku ya kwanza kwa kuwa alikuwa safarini nchini Uingereza kuhudhuria Mazishi ya Malkia Elizabeth II.

Lakini alipotokea katika jukwa la Baraza Kuu Jumatano asubuhi, alianza kwa kuishambulia vikali Moscow kwa kuivamia Ukraine, kutishia kutumia silaha za nyuklia, na kusababisha mgogoro wa chakula ulioathiri mataifa mengi Afrika na sehemu nyingine.

Biden alisema hatua ya Rais wa Russia Vladimir Putin kushambulia Ukraine tangu mwezi Februari ni “ukiukaji mkubwa wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa,” akieleza kuwa “mwanachama mashuhuri wa Baraza la Usalama la UN amevamia nchi jirani yake.”

“Majeshi ya Russia yameshambulia shule za Ukraine, vituo vya treni, na mahospitali, na sehemu ya azma ya Moscow ya “kuzima haki za Ukraine za kuwepo kama taifa,” Biden alisema.

Rais wa Marekani aliongeza kusema “Leo, Putin ametoa vitisho vya wazi vya kutumia nyuklia dhidi ya Ulaya.”

Biden alikanusha kauli za Putin kuwa Russia inatishiwa, akiliambia Baraza Kuu “Hakuna aliyeitishia Russia, Hakuna isipokuwa Russia ndiyo imeanzisha vita.”

Pia alisema kuwa ni “njama” ya mpango unaoendelea katika maeneo yanayodhibitiwa na Russia huko kusini mwa Ukraine kuendesha “kura ya maoni” kujiunga na Russia, na kuondoka chini ya himaya ya Kyiv.

Biden alichukua dakika, kisha akasema kwa uhakika “Vita hii ni kuhusu haki za Ukraine kuwepo kama taifa. Hilo lazima likufanya usisimke mwili.”

“Russia imekiuka misingi muhimu ya mkataba wa Umoja wa Mataifa bila aibu,” Biden alisema.

Biden pia alitumia hotuba yake kwenye Umoja wa Mataifa kutoa wito kupanuliwa kwa Baraza la Usalama ili kuwa na wawakilishi kutoka mataifa ya mabara mengine ambayo hayana uwakilishi.

“Marekani inaunga mkono kuongezwa kwa idadi ya wawakilishi wa kudumu na wasio wakudumu katika baraza hilo,” Biden aliliambia Baraza Kuu la UN.

“Hii ni pamoja na kuwepo viti vya kudumu kwa mataifa hayo ambayo tumeyaunga mkono kwa muda mrefu – viti vya kudumu kwa nchi za Afrika, Amerika Kusini na Carribean. Marekani inaahidi kutekeleza kazi hii muhimu,” alieleza.

Rais wa Marekani pia alitangaza ufadhili mwengine wa dola bilioni 2.9 kwa ajili ya kusaidia hatari ya usalama wa chakula duniani iliyosababishwa kwa kiasi fulani na uvamizi wa Russia katika nchi ya Ukraine inayozalisha nafaka .

White House ilisema usambazaji chakua unahatarishwa vibaya sana na “madhara mengi ya majanga, kuongezeka kwa tatizo la hali ya hewa, kupanda kwa gharama za nishati na mbolea, na vita – ikiwemo uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Repoti hii imechangiwa na taarifa za mashirika ya habari Reuters, AFP na taarifa za Baraza la Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG