Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:22

UN yaomba Taliban kuruhusu tena masomo ya wasichana


Wasichana wa shule ya upili Afghanistan kwenye picha ya maktaba
Wasichana wa shule ya upili Afghanistan kwenye picha ya maktaba

Umoja wa Mataifa Jumapili umeomba utawala wa Taliban nchini Afghanistan kuruhusu tena masomo ya shule za upili kwa wanasichana kote nchini, wakati ukikemea marufuku yaliyowekwa mwaka mmoja uliopita na kuyataja kuwa yenye aibu.

Wiki chache baada ya kuchukua hatamu za uongozi Agosti mwaka jana, utawala wa Taliban ulifungua tena masomo ya shule za upili kwa wavulana Septemba 18, lakini ukapiga marufuku masomo hayo kwa wasichana. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, miezi michache baadaye, hapo Machi 23, wizara ya elimu iliruhusu wasichana kurudi shuleni, lakini saa chache baadaye, uongozi wa Taliban ulibatilisha hatua hiyo.

Tangu wakati huo, zaidi ya wasichana milioni 1 wamenyimwa haki ya elimu kote nchini, kulingana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Afghanistan UNAMA. Mkuu wa UNAMA Markus Portzel kupitia taarifa amesema kwamba marufuku hiyo ni aibu na ingezuilika. Ameongeza kusema kwamba ni hatua inayoathiri kizazi kizima cha wasichana nchini Afghanistan.

XS
SM
MD
LG