Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 03, 2024 Local time: 13:28

Wanaharakati waomba UN kushughulikia elimu baada ya janga


Mshindi wa Nobel wa 2014 Malala Yousfzai
Mshindi wa Nobel wa 2014 Malala Yousfzai

Wakati athari kutokana na janga la Covid 19 likichelewesha masomo kwa watoto kote ulimwenguni, wanaharakati  mjini New York Jumatatu wameomba viongozi wa dunia kuweka kipaumbele suala la mifumo ya elimu, pamoja na kurejesha bajeti zilizositishwa kwenye sekta hiyo baada ya janga kutokea.

Wameyasema hayo wakati wa kongamano kuhusu elimu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kabla ya kufanyika kwa mkutano wa baraza kuu la Umoja huo , ambapo viongozi wanatarajiwa kutoa ahadi zao za kuhakikisha kwamba wanafunzi hawabaki nyuma kielimu kuanzia barani Afrika hadi hapa Marekani.

Mshindi wa tuzo ya Nobel mwaka 2014 kutoka Pakistan Malala Yousfzai, ambaye pia ni mjumbe wa amani wa UN wakati wa kikao hicho alisema kwamba miaka 6 iliyopita alisimama tena mbele ya baraza hilo akiomba sauti ya msichana aliyepigwa risasi wakati akitafuta elimu nchini mwake isikilizwe.

Ameongeza kusema kwamba wakati huo viiongozi waliahidi kuhakikisha kwamba kila mtoto anapata elimu kufikia 2030, na kwamba inahuzunisha kuona hatua zilizopigwa. Mwanaharakati wa vijana kutoka Nigeria Karimot Odebode kwa upende wake alisema kwamba hawatachoka hadi pale kila mwanafunzi kutoka kila kijiji ulimwenguni atakapo pata elimu.

XS
SM
MD
LG