Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 10:51

UN yalaani hatua ya Iran kutumia 'nguvu ya dola kupita kiasi' kufuatia kifo cha Mahsa Amini


 Bi Mahsa Amini
Bi Mahsa Amini

Umoja wa Mataifa umelaani kifo cha Mahsa Amini kilichotokea alipokuwa anashikiliwa na polisi wa Tehran, nchini Iran.

Pia imelaani jinsi polisi inavyotumia nguvu kupambana na waandamanaji kutokana na kifo chake.

Kaimu Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Nada Al-Nashif amesema Jumanne kwamba ameshtushwa na kifo cha Amini akiwa kizuizini na kutaka uchunguzi huru ufanyike.

Hasira za wanainchi zinaogezeka huko Iran ambako kwa siku ya nne sasa waandamanaji wanapambana na maafisa wa polisi katika mji mkuu wa Tehran, kwenye baadhi ya vyuo vikuu na mji anakotoka Bi Mahsa wa Mashhad.

Hasira ziliongezeka tangu Ijumaa pale polisi walipotangaza kifo cha msichana huyo baada ya kulazwa hospitali kwa siku tatu kutokana na kupoteza fahamu kufuatia kukamatwa na kikosi maalum cha polisi cha kutekeleza maadili.

Kikosi hicho kinatekeleza kanuni za kuwataka wanawake kufunika kichwa wakiwa hadharani kilichopitishwa mara ya kwanza baada ya mapinduzi ya 1978, lakini kurudishwa tena na utawala mpya.

Chanzo cha habari hii kinatokana na shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG