Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:28

Iran iko tayari kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wa nyuklia wa Umoja Mataifa


Makao makuu ya IAEA huko Vienna Austria, June 7, 2021. Picha na REUTERS/Leonhard Foeger.
Makao makuu ya IAEA huko Vienna Austria, June 7, 2021. Picha na REUTERS/Leonhard Foeger.

Iran siku ya  Jumatatu imeelezea utayari wa kutoa ushirikiano na waangalizi wa nyuklia wa Umoja wa Mataifa – IAEA, ikisema licha ya taifa hilo kuwa na majukumu lakini pia ina haki zake.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Nasser Kanaani amewaambia wanahabari kwamba Iran inatarajia hatua za msingi kutoka shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki na bodi yake ya utawala.

Shirika hilo linaanza mikutano yake Jumatatu katika masuala mapana ya nyuklia ya kidunia ikijumuisha wasiwasi kuhusu program ya Iran. IAEA imeishinikiza Iran kutoa taarifa za kweli kuhusu uwepo wa chembechembe za uranium zilizo tengenezwa na kukutwa katika maeneo matatu ambayo hayakutajwa katika nchi hiyo.

Iran inataka kumalizika kwa uchunguzi ambao ni sehemu ya mazungumzo ya kurejesha makubaliano ya kimataifa ya mwaka 2015 ambayo yaliipatia nchi hiyo ahueni ya vikwazo kwa kubadilishana na kuacha mpango wake wa nyuklia.

XS
SM
MD
LG