Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 21:35

Magazeti ya Iran yamuenzi mwanamke aliyekufa mikononi mwa polisi


Picha ya Mahsa Amini kwenye kurasa za juu za magazeti ya Iran, Jumapili.
Picha ya Mahsa Amini kwenye kurasa za juu za magazeti ya Iran, Jumapili.

Wakati Iran ikiendelea kuomboleza kifo cha mwanamke muda mfupi baada ya kukamatwa na polisi, ukurasa wa kwanza wa gazeti maarufu la Asia uliwekwa jina lake kwa maneno kwamba, "Mahsa jina lako halitasaulika."

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, kikosi maalum cha polisi kinachohakikisha sheria kali za mavazi ya wanawake zinafuatwa, na ambacho kilimkamata Mahsa kwa siku kadhaa, kimepata ukosoaji mkubwa kutokana na utumizi nguvu kupita kiasi.

Kifo cha Mahsa Amini umri wa miaka 22 kimeibua tena mjadala wa kulinda wanawake wanaodaiwa kukiuka sheria kali za kiislamu za 1979, kuhusiana na mavazi ya wanawake. Siku moja baada ya mazishi ya Mahsa, karibu magazeti yote ya Iran yalichapisha picha yake kwenye kurasa za kwanza Jumapili.

Mahsa ambaye ni kutoka mkoa wa kaskazini magharibi wa Kurdistan alikuwa ametembelea jamaa zake mjini Tehran, ambako alikamatwa na kuzuiliwa Jumanne wiki iliyopita. Televisheni ya kitaifa ilitangaza kifo chake Ijumaa baada ya kusemekana kupoteza fahamu kwa siku 3 baada ya kuzuiliwa.

XS
SM
MD
LG