Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:46

Marekani yatishia kuchukua"hatua kali" dhidi ya Russia iwapo itashambulia Ukraine kwa zana za nyuklia


Rais Vladmir Putin wa Russia (Kushoto) na Rais Joe Biden wa Marekani (Kulia)
Rais Vladmir Putin wa Russia (Kushoto) na Rais Joe Biden wa Marekani (Kulia)

Marekani imeionya Russia kuhusu kile ilichokiita "matokeo mabaya" ikiwa itaanzisha mashambulizi ya nyuklia dhidi ya Ukraine.

Mshauri wa usalama wa kitaifa wa Rais Joe Biden, Jake Sullivan, alisema Jumapili kwamba utawala wa Biden utachukua hatua za haraka endapo hilo litatokea.

Sullivan, akizungumza kwenye kipindi cha "Wiki Hii" cha ABC, alisema maafisa wa Marekani wamewaambia maafisa wa Russia kwa faragha kwamba Biden "atajibu bila kusita" ikiwa Rais wa Russia Vladimir Putin ataamuru shambulio la nyuklia, lakini hakufafanua jinsi Marekani ingejibu.

Sullivan alisema Marekani "haitajihusisha na mchezo wa maneno kuhusu ulipizaji kisasi" na Russia. Lakini Sullivan, katika mahojiano tofauti, aliambia kipindi cha "Meet The Press" cha NBC kwamba "Russia inaelewa vizuri kile ambacho Marekani ingefanya katika kukabiliana na matumizi ya silaha za nyuklia nchini Ukraine kwa sababu imeshajieleza bayana kuhusu hatua hizo."

Jibu la Marekani lilikuja baada ya Putin kuashiria uwezekano wa shambulio la nyuklia wiki iliyopita alipowaita wanajeshi 300,000 wa akiba kusaidia kupigana katika uvamizi wake wa miezi saba nchini Ukraine.

Ongezeko hilo la wanajeshi lilikuja baada ya vikwazo dhidi ya Russia, huku wanajeshi wa Kyiv wakitwaa tena maeneo makubwa kaskazini-mashariki mwa Ukraine ambayo Russia ilikuwa imenyakua katika wiki za mwanzo za vita.

Maandamano makubwa ya kupinga kuitishwa kwa jeshi la Putin yamezuka nchini Russia, huku polisi wakiwakamata mamia ya waandamanaji walioshiriki maandamano ya mitaani mjini Moscow na kwingineko.

XS
SM
MD
LG