Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:49

Rais Putin aamuru raia wa kawaida kujiunga na jeshi katika vita vya Ukraine


Rais wa Russia Vladimir Putin akitoa hotuba wakati wa mzozo wa kijeshi kati ya Russia na Ukraine, Septemba 21, 2022. Picha ya Reuters
Rais wa Russia Vladimir Putin akitoa hotuba wakati wa mzozo wa kijeshi kati ya Russia na Ukraine, Septemba 21, 2022. Picha ya Reuters

Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano ameamuru watu kujiunga na jeshi la Russia katika vita vya Ukraine kwa mara ya kwanza tangu vita vya pili vya dunia na kuunga mkono mpango wa kuteka eneo kubwa la Ukraine.

Alionya nchi za magharibi kwamba alikuwa hafanyi utani aliposema kuwa atakuwa tayari kutumia zana zote walizonazo kuilinda Russia.

Katika hatua kubwa kabisa ya kutaka kuongeza vita vya Ukraine tangu uvamizi wa Moscow Februari 24, Putin amefafanua kwa uwazi kabisa uwezekano wa vita vya nyuklia, alipoidhinisha mpango wa kuteka sehemu kubwa ya Ukraine yenye ukubwa wa Hungary, na kutoa wito kwa askari wa akiba 300,000.

“Ikiwa usalama wa mipaka yetu utatishiwa, bila shaka tutatumia njia zote zilizopo kuilinda Russia na wanainchi wetu, huu sio utani,” Putin amesema katika hotuba kwa taifa kwa njia ya televisheni.

Akitaja mfano wa kupanuka kwa muungano wa NATO kuelekea mipaka ya Russia, Putin amesema nchi za magharibi zinapanga kuiangamiza nchi yake, zikijihusisha na uhasama wa nyuklia, kwa madai ya kujadili uwezekano wa matumizi ya silaha za nyuklia dhidi ya Moscow, na kuzishtumu Marekani, Umoja wa Ulaya na Uingereza kwa kuihimiza Ukraine kuendesha operesheni za kijeshi ndani ya Russia.

XS
SM
MD
LG