Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 05:06

Raia wa Russia wapinga kuhusishwa kwenye mapigano ya Ukraine


Polisi wa Russia wa kukabiliana na ghasia kwenye picha ya maktaba
Polisi wa Russia wa kukabiliana na ghasia kwenye picha ya maktaba

Kundi linalofuatilia masuala ya polisi nchini Russia limesema Jumatano kwamba zaidi ya watu 1,300 wamekamatwa kote nchini humo baada ya rais Vladimir Putin kutangaza hatua ya muda ya kuhusisha raia wa kawaida kwenye mapigano nchini Ukraine.

Kundi hilo kwa jina OVD-info limeseama kwamba lilihesabu takriban watu 1,332 wakiwa wamezuiliwa baada ya kuhudhuria mikutano ya hadhara kwenye miji 38 kote nchini, baada ya tangazo la asubuhi kutoka kwa Putin. Maandamano hayo ndiyo makubwa zaidi kuwahi kutokea Russia baada ya yale yaliotokea muda mfupi baada ya tangazo la Moscow kwamba jeshi lingevamia Ukraine mwezi Februari.

Mwandishi wa habari kutoka shirika la habari la AFP aliyekuwa katikati mwa Moscow alisema kwamba takriban watu 50 walizuiliwa na polisi waliokuwa wamevalia sare za kupambana na ghasia karibu na sehemu ya maduka. Hali pia inasemekana kuwa sawa na hiyo kwenye mji uliyokuwa wa kiutawala wa St Petersburg kulingana na wanahabari wa AFP, wakati waandamanaji wakisema maneno kwamba, " hatutakubali kutumwa kwenye vita."

XS
SM
MD
LG