Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 06:46

Rais Joe Biden asema uvamizi wa Russia Ukraine unatishia kusambaa kwa nyuklia


Rais wa Marekani Joe Biden akisikiliza wazungumzaji kabla ya kutoa hotuba kwenye Mkutano wa Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund huko New York, Marekani, Septemba 21, 2022. REUTERS/Leah Millis.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema uvamizi wa Rais wa Russia Valdimir Putin nchini Ukraine unatishia kusambaa kwa majibu ya kinyuklia akiongeza kuwa unatishia kusambaa kwa majibu ya kinyuklia

Rais Biden alitumia sehemu kubwa ya hotuba yake Jumatano katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York kuishutumu Moscow.

“Tuzungumze wazi wazi. Mwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imemvamia jirani yake, ni jaribio kufuta utaifa wa taifa jingine kwenye ramani,” amesema Rais wa Marekani.

Biden alimshutumu Rais wa Russia Vladimir Putin kwa “kuandaa kura ya aibu ya maoni” ili kujiingiza katika sehemu za Ukraine.

Saa kadhaa kabla ya viongozi wa dunia kukutana katika makao makuu ya UN.

Putin alitangaza sehemu ya uhamasishaji wa jeshi lake na kuongeza wasi wasi wa shambulizi la nyuklia.

“Kwa hakika tutatumia kila njoa tuliyonayo. Huu si uongo,” amesema Rais Putin.

Tangazo la Putin limekuja baada ya wanajeshi wa Ukraine kusogea mbele zazidi katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi. Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy alizungumza kwa njia ya video, kiongozi pekee aliyepewa ruhusuma na UN “kuzungumza kwa njia hiyo.

Rais Zelenskyy anasema “uhalifu umekuwa ukitendwa kwa muda hivi sasa, huku kukiwa na vita vinavyoendelea miongoni mwa wanachama wa UN.”

David Bosco wa Chuo Kikuu cha Indiana anasema “Kwa upande wa kidplomasia kwa Ukraine na kwa wanawaounga mkono Ukraine, nadhani hii itasaidia kuulenga mzozo na pia kwa kweli umekuwa na athari ya kuitenga Russia kwa kiwango kikubwa sana kuliko ilivyo walivyotengwa hivi sasa.”

Biden alisema anaunga mkono upanuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa—hatua ambayo wanachama wa kudumu Russia na China wamepinga hilo.

Rais Biden anasema “hii inajumusha viti kwa wanachama wa kudumu kwa mataifa yale ambayo tumekuwa tukiyaunga mkono kwa muda mrefu na viti vya kudumu kwa nchi za Afrika, Latin Amerika na Carribean.”

Kuzungumzia mzozo wa chakula ulimwenguni, Biden alitangaza msaada wa zaidi yad ola bilioni 2.9

Na mchango mkubwa utaelekezwa kwenye Mfuko wa Ulimwengu wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.

“Hiyo ina maana tutafanya kazi na washirika wetu katika bunge kuichangia dola bilioni 6 nyingine kwa Mfuko wa Ulimwengu.”

Rais na mkewe Jill Biden walirejea Washington Alhamisi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG