Mahamat Said Abdel Kani mwenye umri wa miaka 52 anayedaiwa kuwa mwanachama wa kundi lililokuwa linaongozwa na waislamu la Seleka, anatuhumiwa kwa kuwatesa wafuasi wa upinzani wakati nchi ilipokuwa inatumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.
Kani anashutumiwa kumuua kiongozi wa polisi katika mji mkuu wa Bangii mwaka 2013 ambako wafuasi wa rais aliyetimuliwa Francois Bozize waliteswa vibaya.
Mwendesha mashtaka atategemea ushahidi wa watu 43 katika kesi hiyo ambayo inatarajiwa kudumu kwa miezi kadhaa.
Kundi la utetezi la la Bw Said limetoa hoja kwamba linashaka na ushahidi uliotolewa dhidi yake.