Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:38

Jamhuri ya Afrika ya Kati yaanzisha matumizi ya Bitcoin


Picha inayoonyesha sarafu ya mtandao Bitcoin
Picha inayoonyesha sarafu ya mtandao Bitcoin

Jamhuri ya Afrika ya kati imexindua matumizi ya sarafu ya mtandao – Bitcoin, licha ya kuwepo tahadhari ya shirika la fedha duniani IMF, kuhusu matumizi ya sarafu hiyo ya mtandao.

Jamhuri ya Afrika ya kati imekabiliwa na vita vya miongo kadhaa, na ilitangaza mwezi uliopita kuanza kutumia Bitcoin, hatua inayoifanya kuwa nchi ya kwanza Afrika kutumia sarafu hiyo kuwa sarafu rasmi.

Serikali haijatoa taarifa zaidi namna raia wake watakavyotumia sarafu hiyo.

Tayari kuna wavuti umezinduliwa kwa jina SANGO, kuwaezesha waekezaji kujisajili.

XS
SM
MD
LG