Mahakama hiyo yenye majaji na waendesha mashtaka wa kimataifa na wa Jamhuri ya Afrika ya kati, ilianzishwa kuchunguza uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanyika miongo miwili iliyopita.
Vikao vya mahakama vinafanyika mjini Bangui.
Kuanzishwa kwa mahakama hiyo ni hatua ambayo imesifiwa na baadhi ya majaji wanaoheshimiwa sana na kutajwa kama hatua nzuri sana katika kuhakikisha kwamba haki inapatikana kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mingi.
Lakini baadhi ya watu wameelezea mashaka yao kuhusu utendaji wake utakavyokuwa.
Wanaoshitakiwa katika mahakama hiyo ni wanachama wa kundi la wapiganaji la 3R lenye nguvu sana katika Jamhuri ya Afrika ya kati.
Kundi hilo linashutumiwa kwa mauaji ya darzeni ya watu katika sehemu za kaskazini magharibi mwa nchi.
Rais wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, Piotr Hofmanski, ameandika ujumbe wa twiter akiiunga mkono mahakama hiyo maalum