Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 23, 2025 Local time: 11:09

Mahakama ya ICC yaidhinisha mashtaka dhidi ya kamanda wa Seleka Afrika ya kati


Wapiganaji wa kiislamu wa Seleka
Wapiganaji wa kiislamu wa Seleka

Majaji katika mahakama ya uhalifu wa kimataifa ICC, wameidhinisha mashtaka ya uhalifu wa kibinadamu yaliyofunguliwa na waendesha mashtaka wa mahakama hiyo dhidi ya aliyekuwa kamanda wa waasi wa Seleka katika Jamhuri ya Afrika ya kati.

Uamuzi huo unatoa nafasi kwa Mahamat Said Abdek Kain kufikishwa mahakamani na kesi dhidi yake kuanza kusikilizwa.

Mawakili wa Said, ambaye alikamatwa na kupelekwa kwenye mahakama hiyo ya mjini Hague mwezi Januari, wana kazi ya kubaini kwamba hana hatia.

Taarifa ya ICC imesema kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwa mahakama kuamini kwamba Said alikuwa mwanachama wa ngazi ya juu wa muungano wa Seleka, ulitekeleza uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo kuwanyanyasa wafungwa wakati alipokuwa kiongozi wa kundi hilo kati ya mwezi April tarehe 12 na Agosti tarehe 30 mwaka 2013.

Jamhuri ya Afrika ya kati imekuwa katika migogoro ya kivita tangu muungano wa waasi wenye waislamu wengi wanaojulikana kama seleka au muungano wa lugha ya Sango, walipoingia madarakani mwezi Machi mwaka 2013.

Utawala wao wa kiimla umepelekea kubuniwa kwa kundi pingamizi lenye wakristo, ambao wengi wao wanakabiliwa na mashataka katik amahakama ya ICC.

XS
SM
MD
LG