Mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliyoundwa mwaka 2015 kwa ajili ya kuwafungulia mashtaka washukiwa wa uhalifu wa kivita katika Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR) iliwasikiliza washtakiwa wake wa kwanza siku ya Jumatatu.
Mahakama maalum ya jinai chombo mseto cha mahakimu wa ndani na nje ya nchi imekuwa ikijitahidi kwa miaka mingi kukabiliana na vikwazo vya vifaa, ukosefu wa fedha na uhasama wa ndani. Kizimbani kulikuwa na wanachama watatu Issa Sallet Adoum, Ousman Yaouba, na Tahir Mahamat wa kundi la wanamgambo wenye nguvu wanaoitwa 3R ambao wanatuhuiwa kwa mauaji ya wanavijiji 46 kutoka vijiji vya kaskazini-magharibi mwa vijiji vilivyoko Koundjili na Lemouna hapo Mei 21 mwaka 2019.
Kesi yao ilifunguliwa rasmi na kuahirishwa haraka hadi April 25. Kundi la 3R (Return, Reclamation and Rehabilitation) ni mojawapo ya makundi yenye silaha na yana nguvu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) yanaundwa hasa kutoka kabila la Fulani.