Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:01

Mjumbe mpya wa CAR anatoa wito wa kurekebishwa kikosi cha kulinda amani cha UN


Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR) na nchi zilizo jirani nae
Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR) na nchi zilizo jirani nae

Mjumbe mpya wa Umoja wa mataifa kwa Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR) siku ya Jumatano alitoa wito wa kurekebishwa upya kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa ili kuwalinda raia dhidi ya unyanyasaji kutoka pande zote katika mzozo.

Jamhuri ya Afrika ya kati, taifa la pili kwa maendeleo duni duniani kulingana na UN limeharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013 ingawa vimepungua kasi tangu mwaka 2018.

Valentine Rugwabiza katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari katika mji mkuu Bangui alisema ameomba marekebisho kuhusu dhamira ya kikosi chetu.

Alisema jambo muhimu ni kuchukua msimamo thabiti na kuzuia manyanyaso dhidi ya raia kwa msingi wa taarifa za kuaminika. “Tunashuhudia unyanyasaji kutoka pande zote katika mzozo” aliongeza Valentine.

XS
SM
MD
LG