Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:20

Makundi ya upinzani CAR yagoma kushiriki maridhiano ya kisiasa


Ramani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (C.A.R)
Ramani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (C.A.R)

Makundi ya upinzani huko Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR) yalisema Jumapili kwamba hawatahudhuria mazungumzo ya maridhiano ya kisiasa yanayotarajiwa kufunguliwa Jumatatu kutokana na kutengwa kwa makundi ya waasi kwenye mazungumzo hayo.

Nchi hiyo imegubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013 japokuwa Rais Faustin Archange Touadera, Jumanne iliyopita alitoa wito wa maridhiano ya Republican Dialogue alitoa ahadi ya kwanza miezi 15 iliyopita huku upinzani unasema waasi wanahitaji kuwepo mezani.

Vikosi vya upinzani havitashiriki katika mazungumzo yatakayoanza Jumatatu alisema msemaji wa upinzani Nicolas Tiangaye ambaye anawakilisha jukwaa linalowaleta pamoja makundi ya upinzani yasiyo na silaha. Wakati huo huo msemaji wa rais, Albert Yaloke Mokpeme alisema mazungumzo hayo yataanza kama ilivyopangwa Jumatatu licha ya upinzani kujiondoa.

Rais Touadera aliwashtukiza waangalizi kwa kutangaza ghafla mazungumzo hayo katika hotuba kwa njia ya redio na kutoa notisi ya wiki moja kuwajumuisha wapinzani wasio na silaha pamoja na mashirika ya kiraia.

XS
SM
MD
LG