Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:21

China yaapa 'kufanya msako mkali dhidi ya vitendo vya hujuma vinavyofanywa na makundi hasimu'


Wakazi wa Shanghai wakabiliana na wafanyakazi wa kudhibiti virusi vya corona waliovalia nguo za kujikinga na maambukizi huko Shanghai, China katika hii picha iliyopatikana kutoka katika video ya mitandao ya kijamii iliyotolewa Nov. 30, 2022. Kanda ya video iliyowafikia Reuters.
Wakazi wa Shanghai wakabiliana na wafanyakazi wa kudhibiti virusi vya corona waliovalia nguo za kujikinga na maambukizi huko Shanghai, China katika hii picha iliyopatikana kutoka katika video ya mitandao ya kijamii iliyotolewa Nov. 30, 2022. Kanda ya video iliyowafikia Reuters.

Chama tawala cha Kikomunisti nchini China kimeapa “kufanya msako mkali  kwa vitendo vya hujuma vinavyofanywa na makundi hasimu,” kufuatia maandamano makubwa sana ya mtaani yaliyokuwa hayajatokea kwa miongo kadhaa yaliyofanywa na raia waliochoshwa na masharti makali  dhidi ya virusi.

Taarifa kutoka Tume Kuu ya Siasa na Masuala ya Kisheria ilitolewa Jumanne jioni imekuja wakati vikosi vya usalama vikiwa katika maeneo hayo kuzuia maandamano yasitokee tena yaliyofanyika mwishoni mwa wiki huko Beijing, Shanghai, Guangzhou na miji mingine kadhaa.

Wakati taarifa hiyo haikutaja moja kwa moja juu ya waandamanaji, lakini ni taarifa hiyo ni ukumbusho wa azma ya chama kuimarisha utawala wake.

Mamia ya magari aina ya SUV, magari ya abiria na magari ya kivita yakiwa yamewasha taa yalikuwa yameegeshwa katika mitaa ya mji huo Jumatano wakati polisi na vikosi vya kijeshi vikifanya zoezi la kukagua vitambulisho na kupekua simu za mkononi za watu kuangalia picha, programu zilizopigwa marufuku na ushahidi mwingine ambao huenda waliuchukua kwenye maandamano hayo.

Idadi ya watu waliokuwa wamekamatwa wakati wa maandamano na baadae kufuatia hatua zilizochukuliwa na polisi haijulikani.

Taarifa ya tume hiyo iliyotolewa baada ya kikao kilichoendelezwa Jumatatu na kuongozwa na mkuu wake Chen Wenqing, mjumbe wa Kamati Kuu ya wajumbe 24 wa chama hicho, alisema mkutano huo ulikusudia kutathmini matokeo ya mkutano wa chama uliofanyika Oktoba 20.

Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping

Katika kikao hicho, Xi alipewa haki ya kutawala kwa miaka mitano katika awamu ya tatu kama katibu mkuu, ikimwezesha kuwa kiongozi wa maisha wa China, akiwapanga wanaomunga mkono na kuondoa sauti za upinzani.

“Mkutano huo umesisitiza kwamba vyombo vya kisiasa na kisheria lazima vichukue hatua madhubuti kulinda usalama wa taifa na utulivu wa kijamii,” taarifa hiyo imesema.

“Ni lazima tuvisake vikundi vya maadui vinavyojiingiza na kufanya vitendo vya hujuma kulingana na sheria, tuhakikishe tunawasaka wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa sheria na uhalifu unaovuruga utartibu wa kijamii na kuendelea kudhibiti hali ya utulivu wa k jamii,” ilisema.

Lakini, ikiwa ni chini ya mwezi mmoja baada ya kilichoonekana kama kujihakikishia mustakbali wake wa kisiasa na kutoweza kupingwa, Xi, ambaye ameonyesha ishara ya kupendelea utawla thabiti kuliko chochote kile, anakabiliwa na changamoto kubwa ya umma anaouongoza.

Yeye na chama bado hawajakabiliana moja kwa moja na ghasia, ambazo zimeenea katika vyuo vikuu na mji wa kusini wa Hong Kong wenye utawala kiasi, na pia masikitiko kwa waandamanaji wa China yanayojitokeza kwenye maandamano ya nje ya nchi.

Waandamanaji wengi walilenga kero lao katika sera ya “kutovumilia COVID” ambayo imewafanya mamilioni ya watu kuwa chini ya katazo la kutoka nje na karantini, ikiwazuilia kufikia huduma za chakula na dawa huku uchumi ukiporomoka na kudhibiti vikali safari zote. Wengi walikuwa wanakebehi msimamo wa serikali ambao sababu zake haziishi kubadilika, na pia madai kuwa “maadui kutoka nje” ndiyo wanachochea wimbi hilo la hasira.

XS
SM
MD
LG