Katika kikao na waandishi wa habari, msemaji wa baraza la usalama wa kitaifa John Kirby, amesema kwamba watu wa China wanastahili kuruhusiwa kuandamana kwa amani.
Waandamanaji wanataka amri za kuwazuia kutoka nyumbani kwao kuondolewa, na wamesikika pia wakitaka utawala war ais Xi Jingping kuondoka madarakani na chama chake cha kikomunisti.
Masharti makali ya China namna ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona, yamepelekea kupungua kwa idadi ya vifo ikilinganishwa na Marekani.
Kuna wasiwasi kwamba maandamano ya China yanaweza kuathiri usafirishaji wa bidhaa kutoka China hadi kwa soko la kimataifa, huku chama cha Republican kikitaka utawala wa Joe Biden kuchukua hatua hali dhidi ya maafisa wa chama cha kikomunisti, wanaowadhulumu waandamanaji.