Ni maandamano yasiyo ya kawaida kuonyesha kukasirishwa na utawala wa nchi hiyo.
Waandamanaji wamepaaza sauti zenye ujumbe wa kutaka marufuku ya watu kutoondoka nyumbani kwao kuondolewa.
Watu kadhaa wamekamatwa na kuzuiliwa na polisi.
Maandamano yamefanyika siku chache baada ya watu 10 kufariki katika tukio la moto katika jengo la gorofa linalokaliwa na watu mjini Urumqi, Alhamisi. Kuna wasiwasi kwamba huenda masharti ya watu kutoondoka nyumbani kwao, ilizuia wazima moto kuwaokoa watu, sawa na baadhi ya watu kutojiokoa kwa haraka.
Urumqi umekuwa chini ya amari ya watu kusalia nyumbani kwao tangu mwezi Agosti. Unaripoti karibu visa 100 vya maambukizi ya Covid kila siku.
Watu 40,000 wamethibitsihwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini China, Jumamosi.