Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 02:16

Maandamano ya kupinga masharti ya Covid 19 yaendelea China


Rais wa China Xi Jimping

Hata hivyo Jumapili maandamanano yameenea katika mji wa Shangai na miji mingine baada ya malalamiko kuwa yanaweza kuwa mabaya zaidi na kusababisha idadi ya vifo vya moto katika nyumba moja ya apartment kaskazinimagharibi.

Mashahidi wanasema Polisi wa Shangai walitumia vipulizi vya pilipili kwa takriban waandamanaji 300.

Walikusanyika Jumamosi usiku kuomboleza vifo vya takriban watu 10 waliokufa katika moto kwenye apartment wiki iliyopita Huko Urumqi katika mkoa wa Xinjiang kaskazinimagharibi.

Picha za video zilizopostiwa kwenye mitandao ya kijamii ambazo zinasemekena zilichukuliwa Nanjiang mashariki, Guangzhou kusini na takriban miji mingine mitano zimeonyesha waandamanaji wakipambana na Polisi huku wakijaribu kuondoa vizuizi vilivyowekwa kwa ajili ya kuzuiya kuingia katika maeneo jirani.

Serikali ya rais Xi Jimping inakabiliwa na hasira kutoka kwa wananchi kutokana na sera yake ya kuwa na Zero – Covid ambayo imepelekea kufungwa kwa shughuli na kuzuiya watu kutembea China huku maafisa wakijaribu kutenga kila kesi .

Baadhi ya waandamanaji walionekana katika Video wakipaza sauti wakitaka Rais Xi kujiuzulu au chama tawala kuachia madaraka.

Hata hivyo viongozi wa chama mwezi uliopita waliahidi masharti hayatakuwa na vurugu kwa sababu wangepunguza Guarantini na masharati mengine lakini hilo halijashuhudiwa.

Wakati huohuo maambukizo mapya ambayo yamepelekea kesi za kila siku kuvuka elfu 30 kwa mara ya kwanza yamesababisha maafisa wa ndani kuweka masharti kwa wakaazi na kulalamikia kuzidi kile kinachoruhusiwa na serikali ya kitaifa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG