Mataifa hayo makubwa yenye ushindani yalilumbana kuhusu masuala tofauti ikiwemo suala la Taiwan, usalama na haki za binadamu, lakini kumekuwepo na juhudi za kupunguza joto la mvutano tangu viongozi wa Marekani na China kukutana wiki iliyopita.
Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping walijaribu kupunguza kutupiana maneno lakini tofauti kati yao zilionekana wazi, na mazungumzo kati ya wakuu wao wa ulinzi yalikuwa kama hayo ya marais.
Afisa wa ngazi ya juu katika wizara ya ulinzi ya Marekani amesema mazungumzo kati ya Austin na Wei kando na mkutano wa mawaziri wa ulinzi huko Siem Reap nchini Cambodia, yalikuwa yenye tija na ya kitaaluma.