Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:22

Maandamano yazuka China kupinga kufungiwa shughuli kutokana na COVID-19


Rais wa China Xi Jimping
Rais wa China Xi Jimping

Umati wa watu uliingia mitaani Ijumaa usiku katika mji mkuu wa Urumq , baada ya hasira kali kutawala kutokana na kufungiwa shughuli kwa muda mrefu , kulingana na video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ya China Ijumaa usiku.

Video zilionyesha watu kwenye uwanja wakiimba wimbo wa taifa wa China wenye maneno “ Inukeni , wale mliokataa kuwa watumwa” huku wengine wakipiga kelele kwamba wanataka kuachiliwa kutokana na kufungiwa shughuli ili kuzuiya kuenea maambukizo ya COVID- 19.

Shirika la habari la Reuters limethibitisha kwamba picha hizo zilichapishwa kutoka Urumqi ambako watu wake milioni nne ambao ni wakaazi wa hapo wamekuwa chini ya marufuku ya kuondoka nyumbani kwao kwa takriban siku 100.

Katika mji mkuu wa Beijing takriban kilomita 2, 700 baadhi ya wakazi walifanya maandamano madogo wakiwashambulia maafisa wa ndani kutokana na masharti ya kutotembea yaliyowekwa huku wengine wakifanikiwa kuwashinikiza kuondoa kabla ya muda maalumu uliowekwa.

XS
SM
MD
LG