Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:57

Afunguliwa mashitaka kwa kuiba taarifa za biashara kupeleka China


Jengo la bunge la Quebec, Canada
Jengo la bunge la Quebec, Canada

Polisi wa Canada wamemfungulia mashitaka ya uahini mfanyakazi wa kampuni moja ya Hydro-Quebec, ya Canada, baada ya kudaiwa kutuma siri za biashara kwenda China.

Yuesheng Wang, mwenye umri wa miaka 35, atafikishwa mahakamani katika mji wa Quebec, Jumanne kukabiliana na mashitaka ya kuiba siri za kibiashara.

Alifanya matendo hayo kwa kutumia kompyuta bila ya kupata ruhusa na kufanya udanganyifu na kutosimamia uaminifu wa utumishi wa umma.

Inspekta wa polisi wa eneo hilo David Beaudoin amesema kikosi cha usalama wa taifa kilianza kuchunguza shauri hilo toka mwezi Agosti baada ya kupokea malalamiko kutoka tawi la shirika la Hydro-Quebec.

Ameongeza kusema kwamba alichukuwa taarifa ili kuinufaisha Jamhuri ya watu wa China ili kupata taaarifa za maslahi ya uchumi wa Canada.

XS
SM
MD
LG