Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:18

Kamala Harris amekutana na Xi Jinping mjini Bangkok


Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris (L) akisalimiana na Rais wa China Xi Jinping pembeni ya mkutano wa APEC mjini Bangkok, Thailand, Nov. 19, 2022. (The White House/Handout via Reuters)
Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris (L) akisalimiana na Rais wa China Xi Jinping pembeni ya mkutano wa APEC mjini Bangkok, Thailand, Nov. 19, 2022. (The White House/Handout via Reuters)

"Makamu wa Rais alibainisha ujumbe muhimu ambao Rais wa marekani, Joe Biden alisisitiza katika mkutano wake wa Novemba 14 na Rais Xi; lazima tudumishe njia za wazi za mawasiliano ili kusimamia kwa uwajibikaji ushindani kati ya nchi zetu"

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amekutana kwa muda mfupi na Rais wa China Xi Jinping, leo Jumamosi pembezoni mwa mkutano wa kilele wa ushirikiano wa kiuchumi wa Asia Pacific mjini Bangkok.

"Makamu wa Rais alibainisha ujumbe muhimu ambao Rais wa marekani, Joe Biden alisisitiza katika mkutano wake wa Novemba 14 na Rais Xi; lazima tudumishe njia za wazi za mawasiliano ili kusimamia kwa uwajibikaji ushindani kati ya nchi zetu," afisa huyo wa White House alisema.

Ujumbe huo huenda ukaenda kinyume na ziara yake katika kisiwa cha Palawan nchini Ufilipino siku ya Jumanne, jambo ambalo Beijing huenda ikiliona kama karipio. Njia ya kisiwa cha Palawan katika South China Sea, kilomita 330 tu mashariki mwa Visiwa vya Spratly inadaiwa kwa kiasi kubwa na China na kwa sehemu na Brunei, Malaysia, Ufilipino, Taiwan na Vietnam.

Harris atakuwa afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani kutembelea Palawan.

XS
SM
MD
LG