Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 09:43

Afrika Kusini : Zuma akataa kuhojiwa na tume inayochunguza vitendo vya ufisadi


Rais wa zamani Jacob Zuma (kati) akifika kuhojiwa mbele ya tume ya taifa inayochunguza tuhuma mbalimbali za ufisadi ndani ya serika na makampuni ya serikali, Johannesburg, Afrika Kusini, Julai 17, 2019.
Rais wa zamani Jacob Zuma (kati) akifika kuhojiwa mbele ya tume ya taifa inayochunguza tuhuma mbalimbali za ufisadi ndani ya serika na makampuni ya serikali, Johannesburg, Afrika Kusini, Julai 17, 2019.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameamua kuacha kufika kuhojiwa mbele ya tume ya serikali inayochunguza vitendo vya ufisadi.

Mawakili wa Zuma wamesema Ijumaa kuwa mteja wao anahisi kuwa amekuwa akihojiwa bila ya kutendewa haki.

“Mteja wetu kutoka mwanzoni ... amekuwa akichukuliwa kama mtu mwenye makosa,” amesema wakili wa Zuma, Muzi Sikhakhane.

Rais huyo wa zamani ametoa maelezo wiki hii katika kile kinachoitwa tume inayotumika “na dola kwa maslahi ya watu fulani

Raymond Zondo, anayeongoza jopo la majaji katika uchunguzi huo, amesema, “Tume hii haijapewa uwezo wa kuthibitisha kesi dhidi ya mtu yeyote, lakini imepewa uwezo wa kuchunguza na kuhoji juu ya baadhi ya tuhuma.”

Zuma amekanusha madai ya ufisadi dhidi yake, akisema alikuwa muhanga wa hujuma mbalimbali zilizoelekezwa kwake kumaliza kisiasa, kumvunjia heshima yake na kumuua.

Zuma alishinikizwa kujiuzulu katika wadhifa wake wa urais mwaka 2018 na chama tawala cha ANC baada ya kuhusishwa na kashfa mbalimbali za ufisadi.

Katika tukio moja, waendesha mashtaka walimtuhumu ametumia dola za Marekani milioni 20 za mfuko wa umma kuboresha makazi yake binafsi.

XS
SM
MD
LG