Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:48

Bunge latarajiwa kupiga kura dhidi ya Zuma -ANC


Waandishi wa habari wakiwa nje ya hoteli ambako ANC inafanya mkutano kuamua hatma ya Rais Jacob Zuma, Pretoria, Africa Kusini, Feb. 12, 2018.
Waandishi wa habari wakiwa nje ya hoteli ambako ANC inafanya mkutano kuamua hatma ya Rais Jacob Zuma, Pretoria, Africa Kusini, Feb. 12, 2018.

Chama tawala Afrika Kusini kimesema kuwa bunge litapiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Rais Jacob Zuma Alhamisi, iwapo kiongozi huyo anayekabiliwa na tuhuma hatokubali kuachia madaraka mara moja.

Paul Mashatile, mweka hazina mkuu wa chama tawala cha ANC, ametangaza mpango huo Jumatano, siku ambayo Zuma alikuwa anatarajiwa kubainisha iwapo atakubaliana na matakwa ya chama chake kwamba aachie madaraka.

“Hatuwezi kuendelea kuachia Afrika Kusini isubiri bila ya majibu,” Mashatile amewaambia waandishi wa habari baada ya ofisi ya Zuma kukanusha taarifa zilizoenea kuwa walikuwa wamepanga muda wa Zuma kutoa tamko.

Viongozi wa ANC waliamua mapema wiki hii kusitisha uongozi wa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 baada ya kushikilia madaraka kwa miaka 9 ambao umegubikwa na tuhuma mbali mbali za ufisadi na kutokua kwa uchumi.

Madai hayo ni pamoja na tuhuma za kuwa Zuma ametumia kiasi cha dola milioni 20 za fedha za umma kwa ajili ya kuboresha nyumba zake binafsi.

Zuma hana shinikizo lolote la kisheria kuachia madaraka, na hata hivyo amekataa shinikizo kubwa la kujiuzulu la zaidi ya wiki moja na mazungumzo yanayofanyika katika chama.

Iwapo kura ya kutokuwa na imani naye itapitishwa, Rais wa ANC Cyril Ramaphosa atachaguliwa na bunge kuwa rais mpya wa Afrika Kusini kati ya Alhamisi au Ijumaa.

XS
SM
MD
LG