Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 18:00

Familia ya Gupta yadaiwa kuwa na mafungamano na Zuma


Rais Jacob Zuma

Polisi wamefanya upekuzi katika nyumba ya familia tajiri ya wahindi waliozaliwa India ambao wanamafungamano makubwa na Rais Jacob Zuma.

Kikosi mahiri cha wapelelezi ambao wanajulikana kama Hawks waliwakamata watu watatu katika msako huo kwenye eneo la nyumba ya familia ya Gupta katika eneo la kifahari mjini Johannesburg.

Televisheni ya Taifa SABC imesema mmoja wa wanafamilia wa Gupta ni kati ya wale waliokamatwa.

Familia ya Gupta inatuhumiwa kutumia urafiki wao na Zuma kufanya maamuzi ya uteuzi wa viongozi na mambo mengine.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG