Upatikanaji viungo

Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 21:36

Zuma akabiliwa na kesi ya rushwa


Rais wa zamani Jacob Zuma

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma atakabiliwa na kesi ya rushwa inayohusisha mkataba wa silaha wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2.5 ambao ulisainiwa mwisho wa mwaka 1990, amesema mwendesha mashtaka mkuu Shaun Abrahams,  Ijumaa.

“Baada ya kulipima suala hili, nafikiria kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kumshtaki Zuma kwa makosa yaliyo orodheshwa anayotuhumiwa kwayo,” amesema Abrahams.

Hata hivyo Zuma amekanusha tuhuma zote, amesema Abrahams.

Chanzo cha habari kimeripoti kuwa Zuma anatuhumiwa kutaka rushwa kwa nia ya kujinufaisha kifahari yeye binafsi.

Mshauri wake wa fedha wakati huo alikutwa na hatia ya kuomba rushwa hizo mwaka 2005 na Zuma alimfukuza kazi.

Zuma alifutiwa mashtaka hayo muda mchache kabla ya kuwa rais mwaka 2009.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG