Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:02

Shinikizo la kujiuzulu Zuma lagonga ukuta


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekataa kuachia madaraka baada ya chama chake kumtaka ajiuzulu vyombo vya habari vimeripoti nchini humo.

Zuma amekuwa akikabiliwa na shinikizo ajiuzulu kufuatia mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu katika chama chake cha ANC siku ya Jumapili. Hata hivyo haikufahamika mazungumzo hayo yalijiri katika masuala gani.

Rais Zuma aliwahi kufungwa baada ya kushiriki katika harakati za kutokomeza ubaguzi wa rangi wakati wa ukombozi wa Afrika Kusini. Hivi sasa yuko katika awamu ya pili ya urais wake.

Julius Malema, kiongozi wa upinzani na aliyekuwa mfuasi wa chama hicho cha ANC alisema kwenye mtandao wake wa Twitter kwamba Rais Zuma amekataa kujiuzulu.

Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa katika habari zilizoenea ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa katika mkutano wa Jumapili Zuma aliomba kupata kinga dhidi ya kushtakiwa yeye na familia yake.

Cyril Ramaphosa aliichukuwa nafasi ya kiongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Zuma, anayekabiliwa na tuhuma za rushwa.

Wachambuzi wakisiasa wanasema kuwa wakuu wa chama hicho wanajaribu kuondoa mvutano ambao unaweza kukigawanya chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.

XS
SM
MD
LG